Friday 29 May 2015

SHERIA YA USIMAMIZI YA MAZINGIRA(EMA-2004)

Mchango wangu wa kwanza kwa kifupi ningependa nikujuze kuhusu sheria ya mazingira ya Tanzania.watanznaia wengi wetu hatupendi kujua au kusoma sheria mbalimbali zinazohusu maisha yetu ya kila siku.kama sheria nyingine zilivyo,sheria hii imeandikwa kwa kiingereza na kutafisiriwa kwa kiswahili. Sheria hii ilitungwa mwaka 2004 na kuanza kazi mwezi julai 2005.

Sheria hii inatoa mamlaka mbalimbali kuanzia kwa waziri,Mkurugenzi wa
mazingira,baraza la hifadhi na usimamiz wa mazingira(NEMC),wizara zakisekta,mamlaka za serilkali za mitaa,maafisa mazingira wa ,wilaya,miji,jiji n.k.Pia inaongelea uandaaji na usimamizi mipango wa mazingira yakiwemo;hifadhi na ulinzi,maeneo ya Mazingirwa lindwa.

Sheria hii inatoa muongozo wa shughuli zote zihusuzo mazingira na kwa sasa inatambulika kama sheria mama kwa mambo yote yahusuyo mazingira na ni itatumika kwa mambo yote ya mazingira iwapo sheria nyingine itakinzana nayo.(sura232)

Nakala za sheria hii zinapatikana kwenye duka la serikaili.Tafadhali jipatie nakala yako kwa uelewa ili tuweze kutunza mazingira yetu Tanzania.